• No results found

MRSA – aina ya kimelea sugu kabisa Patientinformation

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2022

Share "MRSA – aina ya kimelea sugu kabisa Patientinformation"

Copied!
2
0
0

Loading.... (view fulltext now)

Full text

(1)

Patientinformation

Kontakta oss

Telefon 0455-73 10 00

Sjukvårdsrådgivning på telefon 1177

www.ltblekinge.se 1177.se/blekinge landstinget.blekinge@ltblekinge.se

Swahili MRSA

MRSA – aina ya kimelea sugu kabisa

Vimelea vimepatikana kwenye zalisho linatoka kwako ambavyo ni sugu kwa viuavijasumu fulani vinavyojulikana kwa majina kamili "MRSA.”

MRSA ni nini?

MRSA inamaanisha Staphylococcus Aureus iliyo sugu kwa Methicillin. Staphylococcus aureus (S.

aureus) ni vimelea vinavyopatikana kwa kawaida kwenye ngozi na tando za makamasi za wengi.

80 % ya idadi ya watu wana S. aureus na takriban 20% wana kimelea hiki puani kimahususi. Ni jambo la kawaida kuvibeba vimelea hivi bila kuwa mgonjwa, hata hivyo, kwa wakati mwingine, huwa vinaweza kusababisha maambukizi ya vidonda, usaha ama maambukizi mengine sugu kabisa. Hata hivyo, vimelea hivi "hukolea" zaidi wakati ngozi ya mtu ina jeraha ama wakati kuna chombo geni, kama tubu ya mkojo iliyowekwa mwilini.

Tofauti iliyopo baina ya S. aureus ya kawaida na MRSA ni kuwa MRSA ni sugu kwa aina za kawaida za viuavijasumu, kitu ambacho kinasababisha maambukizi ya MRSA kuwa ngumu kutibiwa. Ikiwa una vimelea vya MRSA bila kuwa mgonjwa huhitaji kutibiwa.

MRSA inapitishwa vipi?

Ni nadra sana kwa aliye na MRSA kuambukiza wengine. Ikiwa una vidonda vilivyo wazi, eczema- ugonjwa wa ngozi kukauka, kuwa na malengelenge yanayowasha na kuvuja damu yanapopasuka au maambukizi ya ngozi, hii huongeza hatari ya kuwaambukiza wengine. Huenda hatari ikawepo katika hali hizi. Hatari pia huwepo iwapo una tubu iliyowekwa mwilini au njia ya kuunganisha sehemu fulani ya ndani ya mwili na mazingira ya nje. Vimelea huongezeka sana katika hali hizi.

Staphylococci ya kawaida na MRSA zinaweza kusambaa katika hali ya huduma ya afya, hasa katika hali ya kuishi kwa usaidizi fulani wa kipekee au hali zingine za kimatibabu. Usambazaji wa

maambukizi hutendeka pia katika maisha yetu ya kila siku.

MRSA hupatikana kwa sana katika mazingira ya huduma ya afya katika nchi nyingi. Kwa hivyo, hatari ya maambukizi kutoka kwa watu wa kigeni ni kubwa mno.

Je, jukumu la aliye na MRSA ni lipi?

Lazima uwe msafi hasa mikononi.

Hakikisha umetumia choo chako na vifaa vyako vya chooni.

Ikiwa una vidonda vilivyo wazi au eczema hakikisha kuwa hugusi gusi vitu au watu kwenye mazingira ya umma.

Ikiwa una sababu za hatari kuwepo (vidonda vilivyo wazi, eczema, maambukizi ya ngozi, tubu ya mkojo iliyowekwa mwilini, njia ya kuunganisha sehemu fulani ya ndani ya mwili na mazingira ya nje) hakikisha:

 Umeoga ukitumia mfereji ya kuogea bali si jibakuli la kuogea

 Umefunika vidonda vilivyo wazi na bendeji au vifunika vya kimatibabu ikihitajika

 Hakikisha tubu iliyowekwa mwilini iko ndani ya nguo zako

 Daima osha mikono yako vizuri baada ya kugusa tubu iliyowekwa mwilini au kidonda kilicho wazi

(2)

Ukizingatia yaliyo hapo juu, kwa kawaida utaweza kukusanyika na watu wengine.

Msimbo wa Mwenendo kulingana na Fungu la Sheria la Kiswidi la Magonjwa Yanayoweza Kuambukizwa (smittskyddslagen)

Lazima uripoti MRSA kulingana na Fungu la Sheria la Kiswidi la Magonjwa Yanayoweza Kuambukizwa na lazima ufuate mapendekezo na masharti ambayo daktari wako amekuamuru katika mkutano wenu au vipimo ulivyovipokea.

Unapaswa kushiriki katika kufuatilia kusambaa kwa maambukizi na uripoti maambukizi yako ya MRSA unapopokea huduma ya afya, matibabu ya meno au usafishaji wa kimatibabu wa miguu na kucha zake.

Si vizuri kungoja hadi utoboe sehemu fulani ya mwili, uwekewe tojo, ukandwe mwili n.k. ndio ugundue kuwa una sababu fulani za hatari kuwepo.

Je, unaweza kuondoa MRSA?

Ndiyo. Iwapo mazalisho matatu yamepatikana kuwa hasi na huna sababu zingine za hatari kuwepo, daktari anaweza kutupilia mbali taratibu zingine za uchunguzi. Kipindi cha shughuli kama hii hutofautiana kutoka kwa hali moja hadi nyingine.

Watoto walio shuleni au chekecheani

Watoto wanaweza kuenda chekecheani na washiriki katika shughuli zote bora tu wasiwe na sababu za hatari kuwepo. Iwapo kuna sababu za hatari kuwepo, basi mtoto husika anapaswa kubaki nyumbani. Huna jukumu la kuwajuza wafanya kazi wa chekechea ile.

Kwa watoto walio shuleni, hakuna vizuizi mahususi bali tu kuhakikisha kuwa umefuata miongozo ile ya kawaida kwa mtu binfasi. Upigaji ripoti kwa mfumo wa huduma ya afya ya shule huamuliwa kwa ushauri wa daktari wa mtoto husika. Wafanya kazi wengine wa shule hujuzwa inavyohitajika.

Ni jukumu la mlezi/mzazi kuhakikisha kuwa sheria hizi zimefuatwa.

Ikiwa una maswali ya ziada baada ya kusoma maelezo haya, tafadhali wasiliana na mwuguzi anayesimamia MRSA katika Kliniki ya Maambukizi na Ngozi (Infektions- och hudkliniken), simu 0455-73 10 67.

References

Related documents

wako kupiga meno mswaki asubuhi na jioni na dawa ya mswaki iliyo na

Men även om en och annan felaktighet insmyger sig någon gang, far man nog ge Carl Laurin rätt, som en gång när detta tjat på tidningarna åter var framme yttrade: ”Den, som

Keywords: Invisible Disability; Chronic Illness; Young Adult; YA fiction; YA literature; misrepresentation; disability bias; Romanticisation; Miracle Cure; Nicola

Delar av partistödet som överförts till andra delar av partiorganisationen (Vilka motprestationer har erhållits för att stärka partiets ställning i den kommunala

Länsstyrelserna är generellt välvilligt inställda till att göra anpassningar av såväl byggnads innets avgränsning so nivån på skyddsbestä elser för att ta hänsyn

Kielelezo 42. Katika maeneo ya Engaruka jumla ya mahojiano 39 yalifanyika. Kati ya mahojiano hayo, watu 20 walikuwa anaume na 19 walikuwa ni wanawake, na

A lo largo de este capítulo hemos señalado algunas tendencias de nuestro corpus de cuento apocalíptico que lo distingue de lo que la crítica ha escrito sobre la

The results of the study suggest that the contemporary apocalyptic short story in Mexico can be defined by private, individual dramas in the midst of apocalyptic times, giving